Ndugu wanjamii wenzangu nina nia nzuri isiyo na hiyana yeyote ile ya kuanzisha jukwaa hili kujaribu kusahihisha makosa mengi ninayoyaona kila wakati ninaposoma makala za magazeti ya Kiswahili yawe yameandikwa na Watanzania wenzangu au na Wakenya!
Niseme tu, mimi ni msomaji mzuri wa magazeti ya Nipashe, Mwananchi, Taifa leo na Habari leo. na kila ninaposoma huwa nakutana na makosa mengii ya matumizi fasaha ya lugha hii na inanifanya niwe na muamko wa kusaidia kurekebisha matumizi bora ya lugha!
Nina uelewe wa kuwa gazeti la Nationmedia lina utaratibu wa kubadilishana wafanyakazi walio chini ya kampuni mama ya Nationmedia ili tu kubadilishana uzoefu wa matumizi ya lugha mbili zinazotumika na kampuni hii ya habari!
Naomba niwakaribishe Watanzania wote na wale Waswahili wanaodhani wanaweza kusaidia matumizi bora ya lugha hii kwa ufasaha kushiriki katika jukwaa hili!
Karibuni